Luke 19

1Yesu aliingia na kupita katikati ya Yeriko. 2Na hapo palikuwa na mtu mmoja aitwaye Zakayo. Ambaye alikuwa mkuu wa watoza ushuru tena mtu tajiri.

3Alikuwa anajaribu kumwona Yesu ni mtu wa namna gani, lakini hakuweza kuona kwa sababu ya umati wa watu, kwa kuwa alikuwa mfupi wa kimo. 4Hivyo, alitangulia mbio mbele za watu, akapanda juu ya mkuyu ili aweze kumwona, kwa sababu Yesu alikaribia kupita njia hiyo.

5Wakati Yesu alipofika mahali pale, aliangalia juu akamwambia, ‘Zakayo, shuka upesi, maana leo ni lazima nishinde nyumbani mwako.’ 6Akafanya haraka, akashuka na kumkaribisha kwa furaha. 7Watu wote walipoona hayo, wakalalamika, wakisema, ‘Amekwenda kumtembelea mtu mwenye dhambi.’

8Zakayo akasimama akamwambia Bwana, Tazama Bwana nusu ya mali yangu nawapa maskini, na ikiwa nimemnyang’anya mtu yeyote kitu, nitamrudishia mara nne. ‘ 9Yesu akamwambia, ‘Leo wokovu umefika katika nyumba hii, kwa sababu yeye pia ni mwana wa Ibrahimu. 10Kwa maana Mwana wa Mtu amekuja kutafuta na kuokoa watu waliopotea. ‘

11Waliposikia hayo, aliendelea kuongea na alitoa mfano, kwa sababu alikuwa karibu na Yerusalemu, na wao walidhani ya kuwa ufalme wa Mungu ulikuwa karibu kuonekana mara moja. 12Hivyo akawaambia, ‘Ofisa mmoja alikwenda nchi ya mbali ili apokee ufalme na kisha aurudi.

13Aliwaita watumishi wake kumi, akawapa mafungu kumi, akawaambia, ‘fanyeni biashara mpaka nitakaporudi.’ 14Lakini wananchi wake walimchukia na hivyo wakatuma wajumbe waende kumfuata na kusema, ‘Hatutaki mtu huyu atutawale.’ 15Ikawa aliporudi nyumbani baada ya kufanywa mfalme, akaamuru wale watumishi aliokuwa amewaachia fedha waitwe kwake, apate kujua faida gani waliyoipata kwa kufanya biashara.

16Wa kwanza akaja, akasema, `Bwana, fungu lako limefanya mafungu kumi zaidi. ‘ 17Huyo Ofisa akamwambia, Vema, mtumishi mwema. Kwa sababu ulikuwa mwaminifu katika jambo dogo, utakuwa na madaraka juu ya miji kumi. ‘

18Wa pili akaja, akasema, ‘Bwana, fungu lako limefanya mafungu matano.’ 19Huyo Afisa akamwambia, ‘Chukua mamlaka juu ya miji mitano.’

20Na mwingine akaja, akasema, `Bwana hii hapa fedha yako, ambayo niliihifadhi salama katika kitambaa, 21kwa maana niliogopa kwa sababu wewe ni mtu mkali. Unaondoa kile usichokiweka na kuvuna usichopanda. ‘

22Huyo Ofisa akamwambia, ‘Kwa maneno yako mwenyewe, nitakuhukumu, ewe mtumishi mbaya. Ulijua kwamba mimi ni mtu mkali, nachukua nisichokiweka na kuvuna ambacho sikupanda. 23Basi, mbona hukuweka fedha yangu katika benki, ili nikirudi niichukue pamoja na faida?

24Ofisa akawaambia watu waliokuwa wamesimama hapo, ‘Mnyang’anyeni hilo fungu na kumpa yule mwenye mafungu kumi.’ 25Wakamwambia, `Bwana, yeye ana mafungu kumi. ‘

26‘Nawaambia, kila mtu ambaye anacho atapewa zaidi, lakini ambaye hana, hata kile alicho nacho kitachukuliwa. 27Lakini hawa maadui zangu, ambao hawakutaka niwe Mfalme wao, waleteni hapa na kuwaua mbele yangu. ‘’

28Baada ya kusema hayo, aliendelea mbele akipanda kwenda Yerusalemu.

29Ikawa alipokaribia Bethfage na Bethania, karibu na mlima wa Mizeituni, aliwatuma wanafunzi wake wawili, 30akisema: `Nendeni katika kijiji cha jirani. Mkiingia, mtakuta mwana-punda hajapandwa bado. Mfungueni, mkamlete kwangu. 31Kama mtu akiwauliza, `Mbona mnamfungua? ‘Semeni, “Bwana anamhitaji. ‘’

32Wale waliotumwa wakaenda wakamwona mwana-punda kama Yesu alivyokuwa amewaambia. 33Walipokuwa wanamfungua mwana punda wamiliki wakawaambia, ‘Kwa nini mnamfungua mwana punda huyu?’ 34Wakasema, `Bwana anamhitaji. ‘ 35Basi, wakampelekea Yesu, wakatandika nguo zao juu ya mwana punda na wakampandisha Yesu juu yake. 36Alipokuwa akienda watu wakatandaza mavazi yao barabarani.

37Alipokuwa anateremka mlima wa Mizeituni, jumuiya yote ya wanafunzi wakaanza kushangilia na kumtukuza Mungu kwa sauti kubwa, kwa sababu ya mambo makuu waliyoyaona, 38wakisema, ‘Ndiye mbarikiwa Mfalme ajaye kwa jina la Bwana! Amani mbinguni, na utukufu juu!’

39Baadhi ya Mafarisayo katika mkutano wakamwambia, Mwalimu, wanyamazishe wanafunzi wako. ‘ 40Yesu akajibu, akasema, `Nawaambieni, kama hawa wakinyamaza, mawe yatapaza sauti. ‘

41Yesu alipoukaribia mji aliulilia, 42akisema, laiti ungelijua hata wewe, katika siku hii mambo ambayo yanayokuletea amani! Lakini sasa yamefichika machoni pako.

43Kwa kuwa siku zinakuja ambapo adui zako watajenga boma karibu na wewe, na kukuzunguka na kukukandamiza kutoka kila upande. 44Watakuangusha chini wewe na watoto wako. Hawatakuachia hata jiwe moja juu ya jingine, kwa sababu haukutambua wakati Mungu alipokuwa anajaribu kukuokoa’.

45Yesu aliingia Hekaluni, akaanza kuwafukuza wale waliokuwa wakiuza, 46akiwaambia, “Imeandikwa, ‘Nyumba yangu itakuwa nyumba ya sala,’ lakini ninyi mmeifanya kuwa pango la wanyang’anyi”.

47Kwa hiyo, Yesu alikuwa akifundisha kila siku hekaluni. Makuhani wakuu na walimu wa Sheria na viongozi wa watu walitaka kumuua, lakini hawakuweza kupata njia ya kufanya hivyo, kwa sababu watu wote walikuwa wakimsikiliza kwa makini.

48

Copyright information for SwaULB